Log in
updated 5:40 PM UTC, Apr 16, 2017

ESCROW: MHIMILI WA BUNGE WAPEWA JUKUMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameielekeza mihimili mikuu ya dola kuwachukulia hatua stahiki wale wote waliohusishwa na kashfa ya Escrow. Akiwahutubia watanzania kupia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Dimond Jubilee jana,  Rais ameuelekeza mhimili wa Mahakama kupitia kwa Jaji Mkuu kujadili na kuona ni hatua zipi zichukuliwe dhidi ya viongozi wa mahakama waliohusishwa.

Aidha, Rais ameutaka mhimili wa Bunge kupitia kwa Spika uone ni hatua zipi za kinidhamu zinazofaa dhidi ya viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge waliohusishwa na sakata hili. Kwa upande wa mhimili wa serikali Rais amesema tayari Mwanasheria Mkuu, jaji Fredrick Werema, ameshajiuzulu mwenyewe. Aidha, amechukua hatua ya kumwajibisha waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka. Ameongeza kuwa uchunguzi unafanyika na hivi karibuni atachukua hatua dhidi ya waliosalia akiwemo waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bwana Eliakimu Maswi.

Media

Last modified onMonday, 05 January 2015 07:44

1149854 comments

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.